Aunt Ezekiel.
BAADA ya kuzagaa taarifa za staa wa filamu nchini Aunt Ezekiel
kujifungua, mwanahabari wetu ametia timu nyumbani kwa Aunt na
kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mrembo huyo bado yu mjamzito na
taarifa za kujifungua si za kweli.
Aunt akiwa na shosti wake Wema Sepetu.
Mitandao mbalimbali ya kijamii imeripoti taarifa za Aunt kujifungua
kuanzia jana huku mingine ikimpongeza na kuweka kipande cha video
kinachomuonyesha mwigizaji huyo akiwa ammbeba mtoto mchanga.
Aunt Ezekiel.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Aunt Ezekiel jana aliweka kipande
cha video akiwa amembeba mtoto mchanga bila kuandika chochote.
Akiongea
na mwanahabari wetu Aunt amesema kuwa , hicho ni kipande cha mojawapo
ya filamu yake aliyocheza siku nyingi. Na taarifa zilizoenea mitandaoni
kuwa kajifungua si za kweli.
Baadhi ya pongezi za mashabiki wa Aunt baada ya kuweka video inayomuonesha akiwa kambeba mtoto.
ConversionConversion EmoticonEmoticon