Waandishi
wa habari wa kigeni, wanadiplomasia, wanaharakati na wasanii mbalimbali
wametiwa mbaroni na polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
wakiwemo waandishi wa habari wa BBC.
Wanaharakati hao, ambao ni
vijana kutoka nchini Burkina Faso, Senegal na Congo, walikuwa na mkutano
na waandishi wa habari kuhusu jukwaa jipya la kijamii.
Mwandishi wa BBC Maud Jullien ametutumia taarifa inayosomwa na Ben Mwang'onda.
Msemaji
wa serikali na ambaye pia ni Waziri wa Habari Lambert Mende amesema
wanaharataki ambao wanaozuiliwa waliletwa ndani ya nchi ili kuongoza
maasi dhidi ya serikali.
Wanaharakati hao ni raia watatu kutoka Senegal , mmoja wa Bukina Faso na wengine 14 raia wa Congo.
Walifumaniwa na jeshi la polisi na kukamatwa wakati wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Duru
kutoka kwa serikali ya Congo zimeambia BBC kwamba watamrejesha nyumbani
afisa mmoja wa ubalozi wa Marekani aliyeshiriki mkutano wa Jumapili.
Ubalozi
wa Marekani mjini Kinshasa umekiri kufadhili mkutano huo ambao
uliwaleta pamoja vijana wanaharakati ili kubadilishana mawazo.
Hata hivyo ubalozi huo haujadthibitisha ikiwa afisa wake Sturr atarejeshwa nyumbani.
BukinaFaso
na Senegal zimeshuhudia maandamano ya raia kuwapinga viongozi
wanaongangania madaraka kinyume cha katiba za nchi hizo.
Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anatarajiwa kukamilisha muhula wake mwaka 2016.
Mapema
mwaka huu zaidi ya watu 40 waliuawa kwenye maandamano ya raia kupinga
mswada ambao ungewezesha Rais Kabila kuongeza muhula wake.
ConversionConversion EmoticonEmoticon