.

Makumi wauawa katika mapigano huko DRC



  • Makumi ya watu wamepoteza maisha yao kufuatia mapigano yaliyotokea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 

    Kanali Felix Basse Msemaji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo (MONUSCO) amesema kuwa, watu wapatao 30 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mapigano ya juma lililopita kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa Patriotic Resistance Force of Ituri. 

    Taarifa ya MONUSCO imebainisha kwamba, 24 kati ya waliouawa katika mapigano hayo ni wanachama wa kundi hilo na waliobakia ni askari wa Congo Kinshasa. 

    Hayo yanajiri katika hali ambayo, eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambalo lina utajiri mkubwa wa madini, daima limekuwa uwanja wa harakati za makundi ya wanamgambo wa Kikongo na waasi kutoka Rwanda na Uganda. 

    Wananchi wa Congo wanayanasibisha machafuko ya mashariki mwa nchi hiyo na tamaa pamoja na uchu wa mashirika ya kigeni wa kutaka kupora utajiri wa maeneo hayo.

Previous
Next Post »