.

Niki Wa Pili na uchaguzi 2015, Ommy Dimpoz video ya wanjera na director Hanscana na idea za video#255 March 16


Msanii Nikki Wa Pili ameamua kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wa Tanzania kushiriki kwenye uchaguzi wa amani, akipiga story kwenye 255 Nikki Wa Pili amesema kampeni hiyo inaenda kwa jina la ‘Uchaguzi kwa Amani 2015’.
Kampeni hiyo imeanza wiki moja iliyopita kwa lengo la kuwaandaa watu kushiriki kwenye uchaguzi wa amani kutokana na vurugu ambazo huwa zinatokea, kampeni hiyo imeungwa mkono na wasanii mbalimbali.
Nikki amesema Kampeni hiyo itaendelea mpaka siku ya uchaguzi.
10411968_741294435969143_4567407232033705800_n 
Star wa single mpya ya ‘Wanjera’ Ommy Dimpoz amefunguka juu ya video hiyo kuonekana na watu wengi walioigiza kama vichaa, Dimpoz amesema alikusudia kufikisha ujumbe kwa njia tofauti kwa sababu video nyingi alizofanya kuwa na vitu vilivyozoeleka.
hanscana 
Baada ya msanii Jux kuachia video yake ya ‘Nikuite Nani’ iliyoongozwa na director Hanscana, kupitia ukurasa wake wa Instagram director Nisher aliweka post ya picha ya video ya Jux pamoja na Joh Makini na kuandika copy& paste halafu baadaye akaifuta.
Kuna story kwamba Hanscana alicopy idea za Nisher, 255 ilimtafuta Hanscana ambae amesema hakuna kitu kama hicho, wala Nisher sio mtu wa kwanza kutumia idea hiyo.
Hanscana amesema Nisher ni kama amepanic, ni muda mrefu hawajakuwa kwenye maelewano mazuri.


Previous
Next Post »