.

OYA UNGEKUWA NA UPUNGUFU WA DAMU NINGEKUONGEZEA LAKINI AKILI…


Inakuwaje masela wangu hapo kitaani? Ni mpango mzima makachaa? Kama vipi wanangu kitaa hii hapana kwikwi. Basi barida!
Tudei nina mizuka f’lani hivi so noo kumbwela. Hivi wanangu ukiona vichwa vinakula msoto hapo kwa fasi ya kitaa unadhani makachaa wanaweza kuwa na fyucha tamu au ndo kama hivyo mafisadi wameshatekiova?
Wanangu kuna pipo hawambonji kisa wanataka uprezidenti wakati wamekulia ushuani wengine mambele na hawajua haso za huku kitaa. Wana mnadhani wapo fea? Daadeki kama vipi tuwapige dauni kwenye uchanguzi ujao.
Oya piga chini mambo ya mapolitiksi dheni tuzame kwenye mastori moo ya kitaa hapa jamvini. Ama nini watu wangu wa nguvu?
Siku bee nilikuwa kwa magrandiparenti. Nilikwenda kuwapa hai nini na nini na kuona laifu linaendaje. Wakati narandaranda kwa kileji aliibuka mtoto mmoko mkare kinoma. Taimu nalefti kileji alikuwa kinda kinoma. Tudei amekuwa bonge la mbebiz hata mimi hanipi tena kitu cha shikamoo badala yake ananipa tano!
Situwesheni laiki hii imenifanya nibilivu kuwa watoto wa kike huwa wanagroo fasta kuliko machalii. Tupa mbali eji yake ndogo bati bodi lake la kikubwa. Ukimuona utadhani mdada mkubwa.
Basi bana, ndani ya eji yake kiduchu ambayo ni miaka ishirini na kitu, tayari amekrosi kwenye ishu za hatari kinoma.
Iko hivi; mtoto anakwenda kwa neimu la Nancy. Unajua mazee kuna uhusiano wa umbo bomba la shori na jina lake? Kama jina lako halimechi na uzuri wako tusilaumiane bati ninachokijua binadamu wote wazuri! Ama nini? Unaruhusiwa kunikosoa ili tusonge fowadi.
Ebana shori alipokuwa kitu cha koleji alimingo na msela mmoko. Mtoto wa mbwa f’lani hivi. Basi bana wakazama kwenye mambo ishu za kikubwa. Fulu malovee mwanzo mwisho.
Katika taimu yote aliyochili na msela ni takriban miaka bee. Taimu yote hiyo walijiachia kinoma. Ndugu, jamaa na washkaji wote walijua kitu na boksi.
Hivi wanangu mnajua kuna hatari sana ya kujitundika na kitu komfotabo kwenye sosho midia? Maana kila kichwa kinajua kuwa f’lani na f’lani wanatoka so siku ya kumwagana inakuwa ni ishu kubwa. Siyo Insta, Feisibuku, Wasapu na Twita kunakuwa kumenuka kinoma.
Basi bana shori akajiachia ileile na jamaa akibilivu kuwa ndo mtu wake. Anakuteli kuwa katika kipindi chote walichochili tugedha shori kachoropoa mara tano akiamini yeye si ndo mai waifu wa msela?
Deizi zikakatika fasta hatare. Siku ya siku jamaa kamteli shori kuwa amepata mkiksi mwingine ambaye amepanga kumpiga kitu cha mereji.
Huwezi kuamini, hata kumpiga chini yenyewe ilikuwa ni kwa kitu cha sms mwanangu. Dah! Aisee noma sana! Sasa shori yupo krosi rodi na tayari jamaa ameshamtepwetesha mtoto mzuri. Unaambiwa hadi vile vifuu pale kwa fasi ya chesti utadhani kandambili za Ashura ndala ndefu.
Mmenisoma wanyama wangu? Oya masela kuna mambo mengine yaani ingekuwa ni upungufu wa damu ningekuongezea lakini upungufu wa akili…imekula kwako!
Machalii jipangeni kozi maumivu ya moyo yanadifa kutoka kichwa kimoko hadi kingine. Kwa info zako kama ukisababisha maumivu kwa mshkaji wako mazee haiwezi kupita drai. Masti na wewe upokee maumivu tena kwa kiwango cha juu zaidi.
Nimemalizia. Kama vipi sii yuu neksti wiki. Nduki!

Previous
Next Post »