.

RONALDO AMFUNIKA MESSI, AWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO …asema ndo kwanza mkoko unaalika mauwa

Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d'Or) 2014 kwa mwaka wa pili mfululizo akiwatupa Manuel Neuer pamoja na mpinzani wake mkuu Lionel Messi.

Ronaldo, 29 alitoa mchango mkubwa kwa Real Madrid mwaka uliopita na kuiwezesha kutwaa mataji ya  Copa del Rey, Champions League, UEFA Super Cup na Club World Cup.
Ndani ya msimu ulipita, Ronaldo akafunga magoli 56 katika mechi 51 alizocheza. Tuzo hii ya Ballon d'Or inakuwa ni ya tatu kwa Ronaldo, mbili akiwa na Real Madrid na moja akiwa na Manchester United.
“Naweza kumuona mama yangu, familia yangu. Napenda kuwashukuru wote walionipigia kura. Kocha wangu, wachezaji wenzangu, rais wa klabu yangu,” alisema Ronaldo wakati akikabidhiwa tuzo hiyo na Thierry Henry.
“Umekuwa ni mwaka usiosahaulika kwangu. Kushinda tuzo hii, tuzo ya aina hii, ni kitu cha kipekee na naweza kusema kuwa nataka kuendelea kufanya kazi kwa kiwango kile kile na kujaribu kushinda mataji zaidi – binafsi na kwa timu – kwa mama yangu na kwa baba yangu ambaye yuko pale akimtazama mwanaye.
“Nataka kuendelea kuwa bora kadri siku zinavyosonga. Napenda kusema kwa Wareno wote kuwa kamwe sikufikiria kushinda tuzo hii mara tatu katika mazingira tofauti.
“Lakini umekuwa ni utashi wangu wa siku zote. Nataka kuwa mmoja wa wachezaji bora wa miaka yote, hiyo inahitaji vitu vingi kwahiyo nawashukuru wote jioni hii ya leo.”
Previous
Next Post »