.

JAMES RODRIGUEZ ASHINDA TUZO YA GOLI BORA LA MWAKA, apiku goli la kichwa la Van Persie World Cup

Kaitka vikorombwezo viliovyoandamana na tuzo ya Ballon d'Or aliyoshinda Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez akatwaa tuzo ya goli bora la mwaka.
Goli hilo la James Rodriguez lilipatikana wakati wa michuano ya Kombe la Dunia ambapo alifunga dhidi ya Uruguay kwa mkwaju mkali wa mita 25.
Alipokea pasi ya kichwa kutoka kwa Abel Aguilar akautuliza kwa kifua kabla ya kuachia shuti kali lililojaa wavuni.
Wengi walitaraji bao la Robin van Persie alilofunga katika Kombe la Dunia kwa kichwa cha mbali akiruka mithili ya Superman ndiyo lingekuwa bao bora la mwaka, lakini kura hazikutosha.

Previous
Next Post »