.

MBUZI WAZIBWA MIDOMO


  • Mbuzi wakiwa wamezibwa midomo.
    Na Dustan Shekidele, Morogoro/Risasi Mchanganyiko
    KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni ubunifu wa hali ya juu, mfugaji mmoja, Msimbe Jonas wilayani Mvomero, Morogoro amebuni mbinu mpya ya kuzuia mbuzi wake kuingia katika mashamba ya wakulima na kula mazao yao.

    Mwandishi wetu aliyekuwa Mvomero vijijini  hivi karibuni alishuhudia Jonas akiwa na mbuzi wake ambao amewatengenezea chombo (plastiki) na kuwafunga midomo yao ili kuwazuia kula mazao katika mashamba ya watu.

    ...Wakiwa na makopo midomoni.
    “Nimebuni mbinu hii ya kuwazuia mbuzi wangu kula mashamba kwa kuwafunika midomo. Huwa naenda nao hivi hadi mbali kabisa na mashamba ya watu, huko nawafungua ili wale majani,  wameshazoea,” alisema Jonas.
    Aliongeza kwamba mbinu hiyo ni nzuri na imemfanya asiwe na wasiwasi anapopitisha mbuzi wake karibu na mashamba ya wakulima.“Baadhi ya wakulima walioona mbuzi wangu wakiwa hivi wamefurahia sana ubunifu wangu huu,” alisema Jonas.
    Hivi karibuni kulizuka mapigano makali wilayani Mvomero kati ya wakulima na wafugaji wa jamii ya Kimasai na yalisababisha mkulima mmoja kupoteza maisha.
    Wakulima nao wakaamua kulipiza kisasi kwa kuchoma moto nyumba za Wamasai zaidi ya 50 na kusababisha hasara kubwa kwa jamii hiyo.

Previous
Next Post »