Sakata la Escrow: Vigogo wa BoT, TRA, Tanesco wapandishwa kizimbani
Posted:2015-01-17 05:40:29 UTC+03:00
Dar
es Salaam. Meneja Misamaha ya Kodi TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa
, Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Roman Urassa na
Mkurugenzi wa fedha BOT , Julius Rutta Angello wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kuomba na
kupokea rushwa ya mamilioni ya fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
Watuhumiwa
hao wanafanya idadi ya waliofikishwa mahakamani kwa kashfa ya miamala
ya Akaunti ya Tegeta Escrow kufikia watano baada ya watumishi wengine
wawili wa umma kufikishwa mahakamani hapo Jumatano iliyopita.
Waliofikishwa
mahakamani hapo ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma aliwekewa kiasi
cha Sh323 milioni kupitia akaunti yake namba 00120102602001.
Mwingine
ni Mhandisi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), Wizara ya Nishati
na Madini, Theophillo Bwakea aliyepokea rushwa ya Sh161,700,000 kupitia
akaunti yake namba 004101102643901.
Mahakama ya Kisutu leo
Washtakiwa
hao wanaokabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na
kifungu cha 15 (1)(a) cha sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya
mwaka 2015, walifikishwa kwa mahakimu wawili tofauti, Hakimu Mkazi
Janeth Kaluyenda na Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka.
Akisoma
hati ya mashtaka katika kesi namba 16 ya 2015 inayomkabili
Kyabukoba, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai mbele ya Hakimu Kaluyenda kuwa
Januari 27, 2014 katika Benki ya Mkombozi wilaya ya Ilala , alipokea
Sh1.6 bilioni kupitia akaunti namba 00110202613801.
Swai
alidai kuwa mshtakiwa huyo akiwa katika Benki ya Mkombozi alijipatia
kiasi hicho cha fedha ambacho ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta
Escrow na kwamba alizipokea kutoka kwa James Burchard Rugemalira
ambaye ni Mshauri huru wa Kitaalam, Mkurugenzi wa VIP Engineering na
Mkurugenzi wa zamani wa IPTL kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni ya
Mabibo Beer Wines and Spirits ambayo ni mali ya Rugemalira
mahakamani kitu ambacho ni kinyume cha sheria.
Alidai
kuwa Julai 15, 2015, mshtakiwa huyo Kyabukoba akiwa katika benki
hiyo ya Mkombozi alipokea rushwa ya Sh161.7 milioni, Agosti 26,2014
alipokea tena rushwa ya Sh 161.7 milioni na Novemba 14, 2014
alijipatia rushwa ya kiasi kingine cha fedha cha Sh161.7 milioni
kupitia kwenye akaunti hiyo, kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni hiyo
ya Rugemalira mahakamani kitu ambacho ni kinyume cha sheria na kwamba
fedha zote hizo ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, Kyabukoba aliyakana na upande wa mashtaka
ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekwisha kamilika na akaomba ipangiwe
tarehe nyingine kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali
(PH).
ConversionConversion EmoticonEmoticon