Dar es Salaam.
Jaribu kufikiria mwimbaji wa nyimbo maarufu kama Safari Siyo Kifo,
Yako Wapi Mapenzi, Nani Kama Mama, Usilie na nyinginezo anapoamua
kutengeneza video na watayarishaji wakubwa Afrika nini kitatokea?
Hiki
ndicho alichopanga kukifanya mwimbaji wa muziki wa dansi ambaye mara
nyingi hupenda kusimama kama ‘solo artist’, Christian Bella kwa ajili
ya kukuza soko la muziki wa dansi Tanzania, akifuata nyayo za wasanii
wa Bongo Fleva.
Bella
amesema kuwa kuanzia Februari mwaka huu, atatengeneza video kubwa
itakayoongozwa na mtayarishaji God Father nchini Afrika Kusini.
“Kwa
nafasi niliyonayo sasa, nikiendelea na video za ‘kitoto’ nitafeli,
natoa wimbo mmoja matata nitakaoanza nao mwaka, mwanzoni mwa Februari
utakuwa tayari.
Namwomba
Mungu mipango yangu iende kama nilivyopanga, ikiwamo kufanya video
kubwajapokuwa zina gharama kubwa na mimi sitaangalia suala hilo, nataka
mafanikio, hivyo lazima nijilipue ili kujitangaza kimataifa,” alisema
Bella.
Bella
alisema kwa sasa ameshatenga kiasi kikubwa cha fedha ili akamilishe
mpango huo, kwani anaamini akitayarisha video kubwa, itakuwa rahisi
kazi zake kuonyeshwa katika televisheni kubwa Afrika kama MTV Base,
Channel O, Trace na kwingineko.
“Najua
gharama yake inaweza kufika kiasi cha Sh68 milioni. God Father ndiye
mtayarishaji nayemlenga kwa sasa, gharama hiyo ni video tu pasipo
kuangalia mambo mengine, ikiwamo usafiri, mavazi na vitu vingine
muhimu,” alisema.
Alisema uamuzi huo umetokana uchunguzi alioufanya pamoja na ushauri kutoka kwa watu kadhaa, wakiwamo wadau wa muziki.
“Mwaka
huu sifanyi kawaida kama miaka iliyopita, kwa sababu tunakoelekea
lazima tuangalie mwelekeo wa dunia, nini kinahitajika ili kufikia
malengo ya kufanya vizuri.
“Ndoto yangu ni kutengeneza pesa, lakini hilo linawezekana kama nitafanya jitihada,” alisema Bella na kuongeza:
“Kwa mfano, leo wamemtambua Diamond Platnumz katika Channel O, Trace, BET kwa sababu ya video kubwa.
Haimaanishi
kwamba Diamond anafanya muziki mzuri kuliko wasanii wote Tanzania
hapana, lakini tunampongeza na kumuunga mkono na kumpa hongera kwa
kuthubutu vitu vikubwa kama hivi, mtu anayeanza na anayefanya vizuri
lazima umpongeze na wewe upite palepale.”
ConversionConversion EmoticonEmoticon