MWANAMITINDO
na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo amekuwa tishio kwa
msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa urembo na
muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini.
Lulu alipotafutwa, hakupatikana.
Mwanamitindo na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo.
Mtandao
mmoja wa hapa nchini umeendesha zoezi la kuweka picha zao kali
zinazowaonesha wote wawili wakiwa na muonekano na picha kali huku
wakiuliza nani zaidi ya mwenzake.Jokate ameibuka mshindi kwa kupigiwa
kura tano huku watu wakimsifia kuwa ni wa kimataifa zaidi ambapo Lulu
alionekana kupigiwa kura na mtu mmoja.
Msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Amani
liliongea na Jokate ambaye aliwashukuru Watanzania kwa kumpenda na
kumpa nafasi lakini aliwasihi kwa kuwaambia kuwa yeye aonavyo wote ni
warembo.“Mimi naona sisi wote ni warembo, nawashukuru Watanzania
walionichagua na kuniona nafaa,” alisema JokateLulu alipotafutwa, hakupatikana.
ConversionConversion EmoticonEmoticon