-
STAA aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’ ameibuka na kumvaa mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’ akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake.
Staa aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’
Mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’.
Matonya alifafanua kuwa picha hiyo alipigwa katika video yake mpya lakini Jide akaichukua na kuiweka mitandaoni pasipo kumuuliza.Matonya akiwa mtungi.“Ile picha aliyoitumia kunidhalilisha ilikuwa ni ya video yangu ya wimbo mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo itatoka hivi karibuni, sasa yeye ameweka mitandaoni na kusababisha watu wanidharau kwa kuona nimelewa chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha namfikisha mahakamani,” alisema Matonya.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jide aliiposti picha ya Matonya akiwa amelala na kusindikiza na ujumbe ulioonesha kama hamjui msanii huyo hali iliyosababisha mashabiki wengi kumsema vibaya Matonya.
.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ConversionConversion EmoticonEmoticon