.

JK AOMBOLEZA KIFO CHA MFALME ABDULLAH




  • THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
    DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
    Telephone: 255-22-2114512, 2116898
    Website : www.ikulu.go.tz              

    Fax: 255-22-2113425


    PRESIDENT’S OFFICE,
          STATE HOUSE,
                  1 BARACK OBAMA ROAD,  
    11400 DAR ES SALAAM.
    Tanzania.
     
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameitumia Saudi Arabia salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud (90) ambaye alifariki jana, Alhamisi, Januari 22, 2015, na kuzikwa leo, Ijumaa, Januari 23, 2015 mjini Riyadh.
    Katika salamu zake kwa Mfalme mpya, Mfalme Salman bin Abdul Aziz al Saud, Rais Kikwete amesema kuwa anaungana na wananchi wa Saudi Arabia na dunia nzima kuomboleza kifo cha kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Saudi Arabia na katika siasa za eneo la Mashariki ya Kati kwa jumla na kwa muda mrefu.
    Ameongeza Rais Kikwete: “Katika miaka yote 10 ya utawala wake tokea 2005 na kabla ya hapo katika miaka mingine 10 wakati anashikilia utawala badala ya kaka yake Mfalme Fahd aliyekuwa anaumwa, Mfalme Abdullah alithibitisha uongozi wa kuwajibika na msimamo thabiti wa kutafuta amani katika Mashariki ya Kati na dunia itaendelea kumkumbuka kwa mchango huo.”
    Amesisitiza Mhe. Rais Kikwete:  “Aidha, sisi katika Tanzania tutaendelea kuenzi juhudi zake kubwa za kujenga na kuimarisha uhusiano wa karibu kati ya nchi zetu,” amesema Rais Kikwete.
    “Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali ninayoiongoza na mimi mwenyewe, nakutumia wewe Mfalme Salman salamu za rambirambi, na kupitia kwako kwa wananchi wote wa Saudi Arabia kwa kuondokewa na kiongozi wao.  Sisi katika Tanzania tunaungana nanyi kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud. Amen.”
    Imetolewa na:
    Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
    Ikulu – Dar es Salaam.
    23 Januari,2015

Previous
Next Post »