Serikali
ya Misri imesema watu kumi na wanane akiwemo Polisi mmoja wameuawa
wakati wa maandamano yaliyofanyika nchini humo wakati wakiadhimisha
miaka minne tangu kuangushwa utawala wa Hosni Mubarak.
Vifo
hivyo vimetokea mjini Alexandria na cairo,Serikali ilipiga marufuku
kuadhimisha kumbukumbu hizo hali iliyosabbaisha vurugu kati ya
Waandamanaji na Polisi.
Zaidi
ya watu 400 pia wanashikiliwa kutokana vurugu hizo.Hata hivyo serikali
ilipiga marufuku tukio hilo linalodaiwa kuwa ni la kumbukumbu ya
maandamano 2011.
Maandamano
hayo ya mwaka 2011 nchini Misri yalikuwa yakiratibiwa na makundi ya
Waislam wenye msimamo mkali ambapo vikosi vya usalama vilishindwa
kuwadhibiti waandamanaji hao
ConversionConversion EmoticonEmoticon